Mwanao anapaswa kuripoti shuleni siku ya Jumamosi, tar. 7 Februari 2015 saa 3 asubuhi.
KARO:
- Mang'ola -- sh. 300,000/- kwa mwaka
- Nje ya Mang'ola -- sh. 400,000/- kwa mwaka
Karo ilipwe kupitia moja ya akaunti zifuatazo:
- Exim Bank – Karatu A/C No. 0120005247 Anna Gamazo SS
- NBC Bank – Karatu A/C No. 045201010908 Anna Gamazo SS
MICHANGO:
Sh. 165,000/- fedha hii kwa ajili ya sare na michango ya uendeshaji. Inalipwa yote siku ya kujiunga.
Sh. 165,000/- fedha hii kwa ajili ya sare na michango ya uendeshaji. Inalipwa yote siku ya kujiunga.
MAHITAJI:
- Mwanafunzi anapaswa kujinunulia sweta jeusi (sio koti na isiwe na kofia) kwa ajili ya kutumia baada ya masomo.
- Raba nyeupe (isiyokuwa na mchanganyiko wa rangi) kwa ajili ya michezo.
- Jozi za kutosha za soksi nyeupe ndefu zinazofika chini ya goti
- Viatu vyeusi vya ngozi (leather shoes) vyenye kufungwa kwa kamba, jozi mbili.
- Shumizi na sidiria nyeupe au fulana nyeupe kwa ajili ya kuvaa ndani ya shati.
- Vipodozi vyovyote (losheni, glycerine, poda, marashi) haviruhusiwi. Aje na mafuta ya mgando (petroleum jelly) pekee
VIFAA VYA KAZI:
- ndoo mbili kwa ajili ya kuogea na kuchotea maji,
- jembe lenye mpini,
- ufagio wa chelewa, na
- ream moja ya karatasi zenye mistari (ikabidhiwe kwa mhasibu siku ya kuripoti)
VIFAA VYA DARASANI:
- Mathematical set (mkebe wa Hisabati)
- Madaftari angalau 10 (inashauriwa kununua counter books angalau zenye quire 2)
- Vifaa vya kuandikia kama vile kalamu, penseli, crayons na rula
- Kamusi ya Kiingereza (unashauriwa kununua “Oxford Basic Engish Dictionary (3rd au 4th ed.)” au “Oxford Student’s Dictionary”) Kamusi za English-Kiswahili hazishauriwi
VIFAA VYA BWENINI:
- Godoro lenye mfuniko la futi 2.5 kwa 6
- Chandarua ya mbu (ya mviringo) ya rangi ya blue pekee
- Taulo moja (rangi yeyote) kubwa na nguo ya usiku moja (night dress)
- Sabuni za kufulia na kuogea za kutosha, mswaki na dawa ya meno na tochi ya kurunzi (tochi ya kuchaji hairuhusiwi). Taa za sola ni bora zaidi.
- Kitenge au kanga kwa ajili ya kujifunga wakati wa kwenda kuoga.
- Sanduku kubwa (tranka) pamoja na mfuko wa safari (begi)
0 maoni:
Chapisha Maoni